Nchi kavu ni sehemu ya uso wa dunia isiyofunikwa na maji kama sehemu za bahari, maziwa au mito[1]. Nchi kavu inaweza kufunikwa na maji kwa muda katika hali ya mafuriko.
Maisha ya kibinadamu pamoja na kiasi kikubwa cha shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, makazi ya watu na uzalishaji wa bidhaa hutokea kwenye nchi kavu.
Sehemu ambako nchi kavu hukutana na magimba ya maji huitwa pwani au ufuko. Mahali mbalimbali hakuna mstari kamili kati ya nchi kavu na gimba la maji hasa penye kanda la kinamasi au matopetope.