Ngao (kwa Kiingereza "Shield") ni silaha ya kujihami ambayo ilikuwa inatumiwa na jamii mbalimbali za Afrika, kama vile Wangoni, Wazulu, Waxhosa na wengineo hata katika mabara mengine.
Ngao zimejengwa tofautitofauti kwa nyakati tofauti pia, hata ngozi za wanyama zilitumiwa, na ukubwa na uzito ulikuwa tofauti pia.
Ngao bado hutumiwa na vikosi vya polisi na jeshi leo. Ngao nyingi sasa hutengenezwa kwa vifaa vya juu, pamoja na elektroniki.
Ngao zinatofautiana na si tu ngao za mkononi, lakini pia nguo, kama vile fulana, glavu na buti.
Pia ngao huonekana kwenye nembo za taifa kama utambulisho kwa nchi nyingine, kwa mfano nchi ya Kenya, Tanzania na kadhalika.