Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Nyotamkia

Njia ya nyotamkia ikizunguka Jua. Mkia huelekea mbali na Jua kila wakati.
Nyotamkia Hale-Bopp jinsi ilivyoonekana mnamo 1997 angani juu ya Kroatia.
Nyotamkia Wild2 ilivyoonekana kwa umbali wa 240 km kwa kamera ya chombo cha angani Stardust.

Nyotamkia (kometi, pia nyota msafiri, shihabu, Kiing. comet)[1] ni gimba dogo la angani linalozunguka Jua kwa njia ya duaradufu yenye sehemu kubwa mbali na Jua na sehemu ndogo karibu na Jua. Pale inapokaribia Jua inaotesha "mkia" unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia". Mkia huu ni hasa mvuke unaong'aa kutokana na nuru inayoakisiwa.

Mwili wa nyotamkia ni mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu. Nyotamkia hutokea katika sehemu za mbali za mfumo wa Jua, ng'ambo ya obiti ya Uranus, katika Wingu la Oort. Ukubwa hauzidi kipenyo cha kilomita kadhaa zikiwa na maumbo tofauti tofauti. Muda mwingi nyotamkia iko mbali na Jua pengine haionekani kwa darubini. Ikifuata njia ya mzunguko na kukaribia Jua kiasi cha kutosha inaanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya Jua. Ikikaribia Jua zaidi sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke na mvuke huu ni kama angahewa ya muda. Sehemu nyingine ya mvuke huachana na nyotamkia yenyewe na kuonekana kama "mkia". Mkia huu unaelekea kila wakati upande usio wa Jua kwa sababu upepo wa Jua unasukuma mvuke upande ule.

Kati ya nyotamkia ni chache tu zinazokaribia kiasi cha kutosha hadi zinaonekana kuwa na mkia kwa macho tu kwa muda wa wiki hadi miezi kadhaa. Zamani ziliaminiwa kuwa ishara kutoka mbinguni au kutoka kwa Mungu zikisababisha wasiwasi na hofu.

  1. Sacleux ana "nyota ya mkia" comète; Knappert 1993 anataja shihabu, shuhubu na nyota msafiri.

Previous Page Next Page






Komeet AF Komet ALS Cometa AN Comēta ANG धूमकेतु ANP مذنب Arabic مزنب ARZ ধূমকেতু AS Cometa AST Kometa AZ

Responsive image

Responsive image