Orodha ya mito nchini Tanzania inaitaja zaidi ya 2,000, lakini hiyo ni baadhi tu.
Imepangwa kwa taratibu mbalimbali kama ifuatavyo:
- kadiri inavyoelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi ama moja kwa moja ama kwa kuchangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, lakini kuna pia mito michache inayochangia Bahari ya Kati kupitia Ziwa Viktoria na mto Naili, na mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika, huku mingine inaishia katika mabonde nchini kama la Ziwa Rukwa;
- kadiri ya mikoa inapopatikana;
- kadiri ya alfabeti.