Pango (kutoka kitenzi "kupanga") au kodi ya kupanga (kwa Kiingereza: lease au rent) ni pesa ambayo inatakiwa kulipwa kwa wakati kadiri ya mkataba kati ya mwenye nyumba au ardhi na anayepanga mali hiyo.
Kwa kawaida, kodi ya nyumba za kuishi au jengo la biashara hulipwa baada ya muda fulani ambao mwenye mali ile na anayekodi wamekubaliana. Kutolipa kodi ili huenda anayepanga akafurushwa nje au akachukuliwa hatua za kisheria kwa kutotimiza wajibu wake katika mkataba waliowekeana na mwenye nyumba. Mwenye mali kwa upande wake anafaa ahakikishe kwamba mahala pale pamefanyiwa ukarabati, anawajibika anapotakikana na mpangaji.