Pango la Noeli (au pango) ni sanaa inayoonyesha jinsi Yesu Kristo alivyozaliwa.
Hiyo ni kadiri ya desturi za Karne za Kati, ambazo asili yake ni Fransisko wa Asizi (1182-1226).
Ndiye aliyeandaa pango hai akitumia watu na wanyama hai ili yeye na watu wa Greccio wajisikie zaidi washiriki wa tukio la usiku wa Noeli (1223).
Kabla yake picha na sanamu za uzazi wa Yesu zilikuwa zinahusu zaidi maadhimisho ya liturujia kuliko uhalisia wa tukio la Bethlehemu.
Kumbe Fransisko, aliyewahi kuhiji katika Nchi takatifu ya Israeli, alipenda hata wasiofika huko waelewe zaidi hali ilivyokuwa.