Papa Damaso I (takriban 304 – 11 Desemba 384) alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Oktoba 366 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Italia. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Damasus.
Alimfuata Papa Liberius akafuatwa na Papa Siricius.
Kati ya magumu ya nyakati zake, aliitisha sinodi mbalimbali ili kutetea imani ya Mtaguso wa kwanza wa Nisea dhidi ya mafarakano na uzushi.
Pia alimuagiza Jeromu kutafsiri katika Kilatini vitabu vitakatifu vya Biblia ya Kikristo, naye mwenyewe aliheshimu makaburi ya wafiadini kwa kuyapamba kwa mashairi [2].
Mchango wake mkubwa zaidi ni kuthibitisha kanuni ya Biblia kama ilivyo hadi leo katika Kanisa Katoliki.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni 11 Desemba.[3].