Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Papa Simako

Mozaiki ya Papa Simako.

Papa Simako (kwa Kilatini: Symmachus) alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Novemba 498 hadi kifo chake tarehe 19 Julai 514[1]. Alitokea Sardinia, Italia[2] akaja kubatizwa Roma.

Alimfuata Papa Anastasio II akafuatwa na Papa Hormisdas.

Kwa muda mrefu alipaswa kukabili upinzani mkali wa antipapa Laurentius[3][4][5] na wafuasi wake wengi[6].

Alikomboa Wakristo waliofanywa watumwa na Wavandali na kusaidia waliokimbia dhuluma yao.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kwenye tarehe ya kifo chake[7].

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. Hughes, Philip (1947). A History of the Church. Juz. la 1. Sheed & Ward. uk. 319. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2018.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Davis 1989, p. 43f; The original Latin in Mansi 1762, p. 301: quod tandem aequitas in Symmacho invenit, et cognitio veritatis
  5. Despite Laurentius being classed as an antipope, it is his portrait that continues to hang in the papal gallery in the Church of St. Paul's, not that of Symmachus.
  6. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91644
  7. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Previous Page Next Page