Paradiso (kwa Kigiriki παράδεισος paradeisos kutoka Kiajemi cha zamani: پردیس, *paridayda- "eneo lililozungukwa na uzio" au bustani) ni jina la mahali pa amani kamili palipo tarajio kuu la waumini wa dini mbalimbali. Dini za Abrahamu zinatumia jina hilo la Edeni / Paradiso, linaloonyeshwa katika Kitabu cha Mwanzo cha Biblia kama mahali pa uumbaji wa binadamu, na hivyo kuchukuliwa kama kielelezo cha ulimwengu wa kabla ya dhambi ya asili, na vilevile kwa ule unaotarajiwa kuwepo milele.
Neno "paradiso" limeenea katika lugha nyingi (paradis, paradisus, paradise n.k.). Lilitumiwa katika tafsiri ya Kigiriki ya Biblia kwa kutafsiri neno la Kiebrania "Bustani ya Edeni" (גן עדן Gan Eden)[1]