| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kihispania: Paz y justicia ("Amani na Haki") | |||||
Wimbo wa taifa: Paraguayos, República o Muerte ("Waparaguay, jamuri au mauti") | |||||
Mji mkuu | Asuncion | ||||
Mji mkubwa nchini | Asunción | ||||
Lugha rasmi | Kihispania, Kiguaraní | ||||
Serikali | Jamhuri Mario Abdo Benítez | ||||
Uhuru imetangazwa |
14 Mei 1811 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
406,752 km² (ya 60) 2.3% | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - Msongamano wa watu |
7,012,433 (ya 104) 17.2/km² (ya 204) | ||||
Fedha | Guarani (PYG )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC-3) | ||||
Intaneti TLD | .py | ||||
Kodi ya simu | +595
- |
Paraguay (pia: Paragwai) ni nchi ya Amerika Kusini isiyo na pwani baharini.
Imepakana na Argentina, Brazil na Bolivia.
Jina la 'Paraguay' limetokana na lugha ya Kiguarani na linamaanisha 'kutoka mto mkubwa'. Mto huu mkubwa ni Parana.
Mji mkuu ni Asuncion ulioundwa mwaka 1537 na Mhispania Juan de Salazar.