Pembe ni nafasi kati ya mistari miwili pale ambako inakutana. Mistari huitwa "mikono" ya pembe. Nukta inapokutana ni kipeo au ncha.
Kiwango cha pembe hutajwa mara nyingi kwa nyuzi (alama °). Kiwango cha duara ni 360°. Jumla ya pembe katika pembetatu ni 180°.
Kuna pia vipimo vingine vya kutaja kiwango cha pembe kama vile radiani au gon.