Pembenyingi (pia: poligoni) ni umbo bapa lenye pande tatu au zaidi.
Pembenyingi hutokea kama nukta kwenye ubapa zaunganishwa kwa mistari inayofunga eneo au maeneo ndani yao.
Katika jiometria bapa pembenyingi sahili kabisa ni pembetatu.
Pembenyingi sahili haina mistari inayopandana. Ikipandana huitwa pembenyingi tata.