Ramses II au Rameses Mkuu au Sese (1303 hivi - Julai au Agosti 1213 KK)[1] alikuwa Farao wa Misri miaka 1279–1213 KK, wa tatu katika Nasaba ya 19 ya Misri ya Kale.
Mara nyingi anasifiwa kama Farao bora. Waandamizi wake na Wamisri wa baadaye walimuita "Mzee Mkuu".
Ramses II aliongoza majeshi yake mara kadhaa hadi Asia, ili kusisitiza himaya ya Misri juu ya Kanaani, lakini pia kusini hadi Nubia.
Tena alishughulikia sana ujenzi wa miji n.k. Pia kwa sababu hiyo, wengi wanaona ndiye Farao aliyepambana na Musa kadiri ya Biblia.