Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Rasi Hoorn

Rasi Hoorn ikitazamwa kutoka kusini.
Ramani ya Rasi Hoorn yenyewe.
Mahali pa Rasi Hoorn katika Amerika Kusini.

Rasi Hoorn (kwa Kihispania Cabo de Hornos, kwa Kiingereza Cape Horn) ni rasi katika Chile kwenye sehemu ya kusini kabisa ya Amerika Kusini. Ni mahali ambako maji ya Pasifiki na maji ya Atlantiki hukutana.

Jina linatokana na mji wa Hoorn katika Uholanzi, kwa sababu walikuwa mabaharia kutoka mji ule waliochora rasi hii kwenye ramani mara ya kwanza na kuiteulia jina.

Rasi Hoorn ni ncha ya kusini ya funguvisiwa la Tierra de Fuegos (kwa Kiingereza fireland) ambavyo ni kundi la visiwa linalozunguka sehemu ya kusini ya Amerika Kusini bara.

Kabla ya kujengwa kwa Mfereji wa Panama njia ya rasi Hoorn ilikuwa njia muhimu kwa meli kati ya bahari mbili. Mizigo mingi iliyoelekea Kalifornia, Chile au Peru ilipita huko au kwenye mlangobahari wa Magellan uliopo takriban kilomita 120 upande wa kaskazini.

Rasi Hoorn ilitazamwa kuwa hatari kutokana na baridi, dhoruba kali, ukungu wa mara kwa mara, mkondo wa bahari na kutokea kwa siwa barafu kutoka Antaktiki. Zaidi ya meli na jahazi kubwa 800 ziliharibika huko kwa kuzama au kugonga miamba, na watu zaidi ya 10,000 walikufa katika ajali hizo. Ndiyo sababu ikaitwa "makaburi ya mabaharia".

Leo hii usafiri wa mizigo unapita katika mfereji wa Panama.


Previous Page Next Page






Kaap Hoorn AF Kap Hoorn ALS كايب هورن Arabic كيب هورن ARZ Cabu de Fornos AST Horn burnu AZ Горн (мыс) BE Горн (мыс) BE-X-OLD Хорн (нос) Bulgarian Kab Horn BR

Responsive image

Responsive image