Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Reli

Njia ya reli
Reli ya garimoshi yenyewe
Kituo cha reli mjini Mumbai. Reli ya Uhindi inabeba abiria milioni 17 kila mwaka [1] iko kati ya reli kubwa duniani.[2]

Reli (kutoka Kiing. rail / railroad) ni mfumo wa usafiri wa abiria na mizigo kwa treni zinazotembea juu ya vyuma au pau za feleji. Reli ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi. Kwa maana asilia "reli" ni zile "reli za chuma" au reli za garimoshi ambazo kwa kawaida hutumiwa mbili-mbili kijozi kufanya njia ya reli yenyewe.

Kwa nchi nyingi reli ni mtindo muhimu wa usafiri kwa sababu inarahisisha mwendo wa watu na bidhaa. Ikitumiwa vema gharama zake ni afadhali kuhusu usafiri wa barabarani. Mahitaji ya nishati kwa kiwango cha mzigo ni kidogo kuliko barabarani.[3]

Faida yake ni hasa tabia za njia yake; reli za garimoshi huwa na uso tambarare isiyonyoka kwa hiyo magurudumu ya treni hutembea kwa msuguano mdogo.

  1. http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6287152.stm
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-02. Iliwekwa mnamo 2009-12-03.
  3. Railroad Fuel Efficiency Sets New Record Ilihifadhiwa 4 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.- American Association of Railroads

Previous Page Next Page






Eisenbahn ALS قطار السكك الحديدية Arabic Ferrocarril AST Eisnbauhn BAR Gelžkėlis BAT-SMG Чыгунка BE Чыгунка BE-X-OLD Hent-houarn BR Željeznica BS Ferrocarril Catalan

Responsive image

Responsive image