| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Samoa, Muamua Le Atua" (Kisamoa) "Samoa, Mungu awe mwanzo" | |||||
Wimbo wa taifa: | |||||
Mji mkuu | Pago Pago | ||||
Mji mkubwa nchini | |||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kisamoa | ||||
Serikali Mkuu wa Dola
Gavana |
Donald Trump Lolo Letalu Matalasi Moliga | ||||
Eneo la ng'ambo la Marekani Mkataba wa Berlin wa 1899 Mkataba wa kukabidhi Tutila Mkataba wa kukabidhi Manu'a |
1899 1900 1904 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
199 km² (ya 212) 0 | ||||
Idadi ya watu - 2013 kadirio - 2010 sensa - Msongamano wa watu |
54,719 (ya 208) 55,519 326/km² (ya 38) | ||||
Fedha | US Dollar (USD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-11) not observed (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .as | ||||
Kodi ya simu | +1 684
- |
Samoa ya Marekani (kwa Kisamoa: Amerika Samoa au Samoa Amelika) ni Eneo la ng'ambo la Marekani katika bahari ya Pasifiki upande wa kusini wa nchi huru ya Samoa.
Kuna wakazi 54,719 (wengi wakiwa wametokana na wakazi asili) katika eneo la nchi kavu la km² 199.
Eneo lake ni sehemu ya funguvisiwa la Samoa. Kutokea kwa eneo la pekee kulisababishwa na ukoloni wa karne ya 19 ambako Ujerumani na Marekani zilishindana juu ya visiwa hivyo. Funguvisiwa liligawiwa kwa mkataba wa Berlin wa 1899. Sehemu ya mashariki ikawa upande wa Marekani na sehemu ya magharibi upande wa Ujerumani.
Kwa katiba ya mwaka 1967 Samoa ya Marekani ilipewa madaraka ya kujitawala.
Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa Wakalvini (50%) na Wakatoliki (20%), kama si Wamormoni.