Shayiri (Hordeum vulgare) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Shayiri
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Shayiri (kutoka Kiarabu شعير; kwa Kiingereza: "barley") ni mmea wa familia ya nyasi katika ngeli ya monokotiledoni.
Mbegu au punje za shayiri ni nafaka.
Kihistoria ilikuwa chakula muhimu cha watu, lakini siku hizi hulimwa zaidi kama chakula cha wanyama.
Hata hivyo inaungwa katika mkate na ni sehemu ya chakula cha kawaida cha watu katika nchi za Ulaya ya Mashariki.
Inahitajiwa pia kwa ajili ya vinywaji mbalimbali kama bia au maji ya shayiri inayopendwa huko Japani.
Kwa jumla shayiri inavumilia chumvi katika ardhi kuliko ngano lakini haivumilii baridi kama aina kadhaa za ngano.
Nafasi | Nchi | Mavuno (kwa t elfu) |
Nafasi | Nchi | Mavuno (kwa t elfu) |
---|---|---|---|---|---|
1 | Urusi | 15.773 | 9 | Marekani | 4.620 |
2 | Kanada | 12.133 | 10 | Hispania | 4.448 |
3 | Ujerumani | 11.722 | 11 | Denmark | 3.730 |
4 | Ufaransa | 10.357 | 12 | Poland | 3.461 |
5 | Ukraine | 9.000 | 13 | China | 3.350 |
6 | Uturuki | 9.000 | 14 | Uajemi | 2.900 |
7 | Australia | 6.640 | 15 | Ucheki | 2.280 |
8 | Uingereza | 5.545 | Dunia | 139.044 |