Shehia ni jina kwa kitengo cha kata kwenye visiwa vya Unguja na Pemba nchini Tanzania.
Ni ngazi ya chini ya utawala wa nchi. Mara nyingi huitwa pia kwa jina lake la Kiingereza kama "ward". Shehia iko chini ya wilaya (district) na kila wilaya huwa na shehia kadhaa.
Asili ya jina ni neno "shehe" inayomaanisha mzee mheshimiwa katika mazingira ya utamaduni wa Kiislamu na "sheha" kwa matumizi ya kisiasa Zanzibar.[1]