Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Shemasi

Shemasi wa Kanisa Katoliki huko Polandi akiimba mbiu Exsultet usiku wa Pasaka.
Shemasi wa Kiorthodoksi katika mavazi yake rasmi.

Shemasi (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kigiriki: διάκονος, diákonos[1] maana yake "mtumishi", "msaidizi", "mhudumu", au "mjumbe".[2]) ni kiongozi wa Kanisa anayeunganisha wenye daraja za juu na walei.

Hii ni kwa sababu ushemasi ni daraja ya tatu na ya mwisho katika Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa ya Ukristo. Unatolewa na Askofu kwa kumwekea muumini mikono na kumuombea ili atoe vizuri huduma ya Neno la Mungu, ya liturujia na ya matendo ya upendo. Unaweza kutolewa kwa namna ya kudumu au kama hatua ya kuelekea daraja ya upadri.

Katika Kanisa la Moravian ushemasi ni ngazi ya kwanza ya uchungaji.

Katika historia ya Kanisa mashemasi waliotoa mchango mkubwa, mara nyingi kwa kukamilisha ushuhuda wao kwa kumfia Yesu.

Kati yao maarufu zaidi ni Laurenti Mfiadini, Efrem wa Syria, na Fransisko wa Asizi.

  1. "deacon". The American Heritage Dictionary of the English Language (tol. la 4th). Bartleby. 2000. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-25. Iliwekwa mnamo 2008-08-17.
  2. Liddell, Henry George; Scott, Robert (1889). An Intermediate Greek-English Lexicon. Oxford: Clarendon Press. ISBN 0-19-910206-6. Iliwekwa mnamo 2007-10-18.

Previous Page Next Page






Diakon ALS شماس Arabic ܡܫܡܫܢܐ ARC شماس ARZ Diáconu AST Дыякан BE Дякон Bulgarian পরিচারক Bengali/Bangla Diagon BR Đakon BS

Responsive image

Responsive image