Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Siku ya Bwana

Ishara ya Chi Rho ikidokeza ushindi wa Mfufuka, 350 hivi.

Siku ya Bwana (kwa Kigiriki, κυρακή ἡμέρα, "kyurakee eemera"; kwa Kilatini, Dominica dies) ni jina ambalo Wakristo wa lugha mbalimbali wanalitumia kutaja Jumapili.

Jina linapatikana katika kitabu cha mwisho cha Biblia ya Kikristo, Ufunuo (1:10).

Chanzo chake ni kwamba ndiyo siku ya juma ambayo wanasadiki Yesu alifufuka kutoka wafu. Hivyo ndiyo mwanzo wa uumbaji mpya wa vyote katika utukufu wake.

Kwa msingi huo, wengi wao wanaiheshimu kama siku muhimu zaidi kwa ibada zao, hasa kwa adhimisho la ukumbusho wake aliloliagiza akiwa katika karamu ya mwisho.

Ushuhuda wa kwanza wa desturi hiyo unapatikana katika Matendo ya Mitume (20:7).

Katika maandishi ya karne ya 2 BK, kwa mfano yale ya Yustino mfiadini, inaonekana desturi hiyo ilivyokuwa imeenea.

Mwaka 361 desturi hiyo iliagizwa rasmi.


Previous Page Next Page






يوم الرب Arabic يوم الرب ARZ Adlaw sa Ginuo CEB Dydd yr Arglwydd CY Tag des Herrn German Lord's Day English Día del Señor Spanish روز خداوند FA Hari Tuhan ID 主日 Japanese

Responsive image

Responsive image