Siku ya nyota (ing. sidereal day) ni mfumo wa kupima urefu wa siku ambao hutumiwa kwa kawaida na wataalamu wa anga. Katika mfumo huu, urefu wa siku hupimwa kama muda ambapo nyota za mbali zinarudia mahali pale pale angani. Muda huu ni tofauti na siku kawaida kwa kuwa mwendo wa Dunia kuzunguka Jua husababisha nyota za mbali kuenda polepole kuliko Jua.