| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Nad Tatrou sa blýska ("Radi juu ya milima ya Tatra") | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Bratislava | ||||
Mji mkubwa nchini | Bratislava | ||||
Lugha rasmi | Kislovakia | ||||
Serikali | Democrasia Peter Pellegrini Robert Fico | ||||
Uhuru kutoka Chekoslovakia |
tarehe 1 Januari 1993 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
49,037 km² (ya 130) -- | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2022 sensa - Msongamano wa watu |
5,424,687 (ya 119) 5,460,185 111/km² (ya 104) | ||||
Fedha | EURO (€ )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .sk2 | ||||
Kodi ya simu | +4213
- |
Slovakia (kwa Kislovakia: Slovensko) ni nchi ya Ulaya ya Kati yenye wakazi milioni tano na nusu.
Imepakana na Ucheki, Austria, Poland, Ukraine na Hungaria.
Slovakia imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.
Mji mkubwa na mji mkuu ni Bratislava.
Miji muhimu baada ya Bratislava ni Košice, Banská Bystrica, Žilina, Trenčín, Nitra, Prešov na Trnava.
Wakazi walio wengi wanasema Kislovakia, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, lakini kieneo kuna pia wasemaji wa Kihungaria, Kibelarus na Kiukraine.
Upande wa dini, 65.8% ni Wakatoliki, 8.9% Waprotestanti. 13.4% wanajitambulisha kama Wakanamungu.