Sulfuri (salfa, kibiriti) | |
---|---|
Sulfuri ikiwaka yayeyuka kuwa kiowevu chekundu; rangi ya moto ni buluu.
| |
Jina la Elementi | Sulfuri (salfa, kibiriti) |
Alama | S |
Namba atomia | 16 |
Mfululizo safu | Simetali |
Uzani atomia | 32.065 |
Ugumu (Mohs) | 2.0 |
Kiwango cha kuyeyuka | 388.36 K (115.21 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 717.8 K (444.6 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.05 % |
Hali maada | imara |
Sulfuri (pia salfa au kibiriti, ing. sulfur) ni elementi simetali yenye namba atomia 16 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 32.065. Alama yake ni S. Kwenye hali sanifu ni imara kuwa fuwele zenye rangi ya njano.