Tako la bara (ing. continental shelf) ni sehemu ya bara iliyoko chini ya maji ya bahari. Sehemu ya bahari hadi ya kina cha maji cha mita 200 huitwa "bahari ya takoni". Kwa wastani lina upana wa 70 – 80 km. Lakini kuna matako yenye upana wa kilomita zaidi ya 1,000 kama huko Siberia au nyembamba sana kama huko Kenya.
Kanda hili la tako lazungusha kila bara. Katika historia ya dunia sehemu hizi ziliwahi kuwa nchi kavu katika vipindi ambako hali ya hewa ilikuwa baridi zaidi na kiasi kikubwa cha maji cha bahari kuwa barafu nchani.
Tako la bahari kwa kawaida huishia kwenye mtelemko ambako sakafu ya bahari unatelemka chini kwa vilindi vya bahari.
Tako la bahari ni muhimu kibiolojia, kiuchumi na kisiasa.