Tani moja ni kipimo cha masi ya gimba ambacho ni sawa na kilogramu 1,000. Si kipimo halisi cha SI lakini hukubaliwa pamoja navyo vipimo sanifu. Kama kipimo sanifu cha SI ingeitwa "megagramu" ambayo haitumiki.
Ni kipimo muhimu katika takwimu za biashara na uchumi.
Neno tani hutumiwa pia kwa kutaja ukubwa wa ngama ya meli lakini hii ni kipimo tofauti si sawa na tani ya SI. Kipimo cha kimataifa kimekuwa tani ya "gross tonnage" au tani GT.