Toscana (ing. Tuscany) ni mmoja kati ya mikoa 20 ya Italia.
Iko katikati ya rasi ya Italia, kaskazini kwa Roma.
Imepakana na mikoa ya Emilia-Romagna, Liguria, Umbria, Marche na Lazio, mbali ya bahari ya Kati.
Eneo lake ni la km² 20,990.
Jumla ya wakazi ilikuwa 3,516,000 mwaka 2004.
Toscana huitwa mkoa mzuri wa Italia kwa sababu ya hali ya hewa, uzuri wa mabonde na milima na urithi wake wa utamaduni na sanaa.