Tuamotu ni funguvisiwa la Polinesia ya Kifaransa. Kiko upande wa kaskazini-mashariki wa kisiwa cha Tahiti. Ni funguvisiwa kubwa kabisa duniani. Mwaka wa 2002, idadi ya watu visiwani imehesabiwa kuwa 15,862. Watu wakaao visiwani kwa Tuamotu huongea Kituamotu na Kitahiti.