Tupac Shakur | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Tupac Amaru Shakur |
Pia anajulikana kama | 2Pac, Pac, Makaveli, MC New York |
Amezaliwa | East Harlem, Manhattan New York City, New York, U.S. | Juni 16, 1971
Amekufa | 13 Septemba 1996 (umri 25) Las Vegas, Nevada, U.S. |
Kazi yake | Rapper, mwigizaji, mtayarishaji wa rekodi, mshairi, mwandishi-skrini, mwanaharakati, mtunzi |
Miaka ya kazi | 1988–1996 |
Studio | Death Row, Interscope |
Ameshirikiana na | Outlawz, Thug Life, Danny Boy, Digital Underground, Dr. Dre, Johnny "J",Ice Cube, Nate Dogg, The Notorious B.I.G., Snoop Dogg |
Wavuti | www.2Pac.com |
Tupac Amaru Shakur (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 2Pac; mara nyingi aliitwa tu Pac, Makaveli na mwenyewe akajiita The Don Kiluminati; 16 Juni 1971 - 13 Septemba 1996) alikuwa mwigizaji, mwanaharakati wa haki za binadamu, na mwanamuziki maarufu wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliouza rekodi nyingi za muziki duniani.
Alikuwa mtoto wa Afeni Shakur, mwanachama wa chama cha Black Panther Party. Mama yake Tupac alitolewa jela mwezi mmoja kabla ya kumzaa Tupac. Tupac alikariki baada ya kupigwa risasi akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada, siku saba kabla ya kifo chake.
Tupac aliwahi kuishikilia Guinness World Record kwa kuwa na mauzo ya juu sana kwa msanii wa muziki wa rap/hip hop. Alipata mauzo takriban milioni 74 kwa hesabu ya dunia nzima na milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee.