Suomen tasavalta (Kifini) Republiken Finland (Kiswidi) |
|||
Wimbo wa taifa "Maamme" (Kifini) "Vårt land" (Kiswidi) ("Nchi yetu" Kiswahili) |
|||
Eneo la Ufini kati Umoja wa Ulaya |
|||
Jiji kubwa (na Mji Mkuu) |
Helsinki | ||
---|---|---|---|
Dini | Ukristo wa Kilutheri na wa Kiorthodoksi | ||
Aina ya Serikali | Bunge la Jamhuri | ||
Rais | Alexander Stubb | ||
Waziri Mkuu | Petteri Orpo | ||
Ukubwa wa eneo | |||
Jumla | 338,145 km² | ||
Asilimia ya Maji | 9.4 % | ||
Idadi ya Watu | |||
Mwaka wa Makisio | 2024 | ||
Idadi ya watu (makisio) | 5,635,560 [1] | ||
Mwaka wa sensa | 2010 | ||
Idadi ya watu (sensa) | 5,375,216 [2] | ||
Msongamano | 16 /km² | ||
Pato la Taifa PPP | |||
Mwaka wa Makisio | 2005 | ||
Jumla | $163 billioni (ya ya 52) | ||
Capita | $31,208 | ||
Pato la Taifa | |||
Mwaka wa Makisio | 2005 | ||
Jumla | $163 billioni (ya ya 52) | ||
Capita | $31,208 | ||
Kiashiria cha Maendeleo ya Watu (2005) | 0.941 (ya 13) Maendeleo ya Juu Sana |
||
Sarafu | Euro (€)1 | ||
Eneo la saa | EET | ||
Nambari ya mwito | +358 |
Ufini (kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.
Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.
Ufini ilijitegemea mnamo 1917. Kati ya 1939 na 1944, Ufini ilipigana dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na jeshi la Ufini liliongozwa na kamanda Carl Gustaf Emil Mannerheim.
Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.