Ugaidi (kutoka Kiar. غيظ ghaiz kwa maana ya hasira[1]) ni hasa mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Watendaji wa ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.
Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapigania uhuru au watu wanaoendesha vita ya msituni. Hata jeshi rasmi ya serikali linaweza kutumia mbinu za kigaidi lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi.