Ukeketaji (pia: tohara ya mwanamke; kwa Kiingereza: female circumcision, female genital mutilation; kifupi: FGM) ni tendo la kukata sehemu za nje za viungo vya uzazi vya mwanamke.
Neno linalotokana na mzizi keket, ambao unabeba maana ya kuharibu.
Mara nyingi tendo la ukeketaji linaitwa pia "tohara" kwa kulifananisha na upasuaji mdogo wa wanaume, lakini mambo ni tofauti kabisa.
Hapa sehemu za nje za viungo vya uzazi zinakatwa kusudi wasifurahie sana tendo la ndoa, hivyo wawe waaminifu zaidi kwa waume wao.
Ukeketaji umeenea hasa kati ya mataifa na makabila wenye asili ya bonde la Naili na majirani wao.
Kinyume na tohara ya wavulana matabibu wanaona hasara nyingi katika desturi hiyo. Ukeketaji unasababisha wasichana wengi kufa na wengine wengi kupatwa na maumivu makali wakati wa hedhi, wa tendo la ndoa na wa kujifungua.
Kwa sababu hizo serikali nyingi za dunia zimeupiga marufuku.
Pia madhehebu kadhaa yanatoa mafundisho kuwa ni kinyume cha masharti ya dini yao.
Juhudi zimefanikiwa kwa kiasi fulani katika baadhi ya nchi.
Kiwango kikubwa sana | Kiwango kikubwa | Kiwango cha wastani | Kiwango cha chini | Kiwango cha chini sana |
---|---|---|---|---|
Somalia 98% |
Gambia 76% |
Guinea-Bissau 50% |
Jamhuri ya Afrika ya Kati 24% |
Iraq 8% |
Guinea 96% |
Burkina Faso 76% |
Chad 44% |
Yemen 23% |
Ghana 4% |
Jibuti 93% |
Ethiopia 74% |
Côte d'Ivoire 38% |
Tanzania 15% |
Togo 4% |
Egypt 91% |
Mauritania 69% |
Kenya 27% |
Benin 13% |
Niger 2% |
Eritrea 89% |
Liberia 66% |
Nigeria 27% |
Cameroon 1% | |
Mali 89% |
Senegal 26% |
Uganda 1% | ||
Sierra Leone 88% |
||||
Sudan 88% |