Makala hii inajadili "Ulimwengu" kama jumla ya vitu vyote; kwa habari za sayari tunapoishi angalia Dunia
Ulimwengu ni jumla ya vitu vyote vilivyopo. Inajumlisha Dunia yetu pamoja na kila kitu ndani yake, jua letu, mfumo wa jua, sayari, nyota, galaksi n.k. Ni jumla ya mata, nishati na anga la Dunia pamoja na anga-nje.