Uzazi ni mchakato wa kibiolojia ambao kiumbe hai kipya kinapatikana kutokana na kingine au vingine.
Uwezo wa kuzaa ni kati ya sifa kuu zinazotambulisha uwepo wa uhai; kila kiumbe hai kilichopo duniani kimetokana na uzazi. Inakadiriwa kwamba kiumbe hai kilichozaa vile vyote vilivyopo leo kiliishi miaka 3,500,000,000 hivi iliyopita.