Valle d'Aosta (kwa Kifaransa:Vallée d'Aoste; kwa Kiswahili: Bonde la Aosta) ni mkoa wenye kujitawala wa Italia. Ni mkoa mdogo kuliko yote kwa eneo (km² 3,263) na kwa idadi ya wakazi (126,935) na kwa sababu hiyo hauna wilaya ndani yake.
Wakazi wengi wanaongea Kiitalia, lakini pia lahaja maalumu ya Kifaransa.