Veracruz (jina rasmi: Veracruz de Ignacio de la Llave) ni moja kati ya majimbo ya Mexiko upande wa mashariki ya nchi. Upande wa mashariki ni maji ya Ghuba ya Meksiko. Mji mkuu ni Xalapa na mji mkubwa ni Veracruz.
Imepakana na Tamaulipas, Oaxaca, Chiapas, Tabasco, Puebla, Hidalgo na San Luis Potosí. Jimbo lina wakazi wapatao 7,110,214 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 71,699.
Gavana wa jimbo ni Fidel Herrera Beltrán.
Lugha rasmi ni Kihispania.