Viro (pia: Wiro, Wera, Vira; karne ya 7 – Roermond, Uholanzi ya leo, 700 hivi) alikuwa mmonaki askofu kutoka Ireland au Britania, maarufu kwa umisionari wake kati ya Wafrisia. Pamoja na wenzake Plekelmi askofu na Odgeri shemasi alianzisha monasteri alimofariki[1].
Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu.