| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Desire the right" | |||||
Wimbo wa taifa: "God Save the Queen" | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Stanley | ||||
Mji mkubwa nchini | Stanley | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Eneo la ng'ambo la Uingereza Elizabeth II wa Uingereza | ||||
Eneo la ng'ambo la Uingereza Siku ya uhuru (Ushindi juu ya Argentina) |
14 Juni 1982 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
12,173 km² (162) 0 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2008 kadirio - Msongamano wa watu |
3,140 [1] (217) 0.26/km² (240) | ||||
Fedha | Falkland Islands pound (FKP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC-3) | ||||
Intaneti TLD | .fk | ||||
Kodi ya simu | +500
|
Visiwa vya Falkland (kwa Kiingereza: Falkland Islands; kwa Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban km 450 mbele ya pwani ya Argentina.
Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.