Voi ni mji mkubwa wa Kaunti ya Taita-Taveta, kusini mwa Kenya. Awali ilikuwa kati ya wilaya sita za Mkoa wa Pwani.
Voi inapatikana Magharibi mwa jangwa la Taru, Kusini na Magharibi mwa Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Magharibi iliyo maarufu sana duniani kote.
Wakazi walikuwa 45,483 wakati wa sensa ya mwaka 2009[1].