Waalur ni kabila la Waniloti wanaoishi kaskazini magharibi mwa Uganda (Wilaya ya Nebbi, Wilaya ya Zombo na Wilaya ya Arua) na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanakadiriwa kuwa 1,735,000 hivi.
Lugha ya wengi wao ni Kialur, mojawapo kati ya lugha za Kiniloti.