Wafinisia (au Wafoinike) walikuwa wakazi wa Finisia ambao zamani za Nyakati za Kale waliishi kwenye mwambao wa mashariki wa Bahari ya Mediteranea.
Miji-dola yao ilikaa katika eneo la nchi za kisasa za Lebanoni na Syria.
Wafinisia walizungumza Kifinisia kilichokuwa lugha ya Kisemiti ambayo ilipotea baada ya kusambaa kwa Kiarabu tangu karne ya 7.
Walikuwa wafanyabiashara na mabaharia hodari sana. Walijenga utajiri wao juu ya biashara ya ubao kutoka milima ya Lebanoni. Hasa miti ya aina ya seda (Cedrus Libani) ilitafutwa sana.
Baadaye waliunda makoloni yao katika magharibi ya Mediteranea hadi Hispania. Lakini koloni lao mashuhuri lilikuwa Karthago (Afrika ya Kaskazini).