Wagermanik (kutoka Kilatini "Germani" kupitia Kiingereza "Germanic people") ni jina la kundi la kihistoria la makabila na mataifa yenye asili ya Ulaya Kaskazini ambayo hujumuishwa kutokana na lugha zao zilizofanana.
Lugha hizo zinazoitwa lugha za Kigermanik ni kundi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za Kigermanik huzungumzwa leo hii na wasemaji wa Kijerumani, Kiingereza, Kiholanzi, Afrikaans, lugha za Skandinavia na nyinginezo, lakini kwa kawaida wasemaji wa leo hawaitwi tena "Wagermanik" bali huangaliwa kama ukoo wa baadaye wa Wagermanik wa kale.