Wameru wa Tanzania (au "Warwa") ni kabila la watu wa Kibantu wa jamii ya Wachaga wanaoishi hasa kwenye Mlima Meru katika Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa nchi ya Tanzania.
Wanakadiriwa kuwa milioni 2, wengi wao wakifuata dini ya Ukristo.
Mbali na jina, Wameru hao ni tofauti kabisa na Wameru wa Kenya kwa historia na utambulisho. Sanasana ni kwamba pande zote mbili ni wakulima wenye bidii kubwa[2].
Inasemekana Wameru walifikia mlima huo miaka 800 hivi iliyopita wakitokea milima ya Usambara, Mkoa wa Tanga. Walikuta huko wawindaji walioitwa Wakoningo ambao walikuja kumezwa na jamii ya Wameru.[3]