Wangulu (au Wanguu) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi mipakani mwa mikoa minne ya Tanga, Dodoma, Manyara na Morogoro, hasa upande wa Kusini-Magharibi mwa mkoa wa Tanga ambako sasa ni wilaya ya Kilindi na upande wa Kaskazini-Mashariki mwa mkoa wa Morogoro ambako sasa ni wilaya ya Mvomero na milima ya Nguu. Upande wa Magharibi ni mkoa wa Manyara ambayo sasa ni wilaya ya Kiteto.
Masimulizi ya kale ya Mbega na Kimweri yanasema kuwa kabila la Wanguu ndilo kabila mama la makabila ya Wazigua, Wabondei, Wasambaa, Waluvu na Wakilindi, ambapo makabila hayo yanaendeleza mila na desturi za asili moja na katika umoja huo hujulikana pia kwa jina moja la Waseuta. Kwa asili Wanguu ni wafugaji na wakulima.