Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Wanyiha

Wanyiha ni kabila la watu wa Tanzania (Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe). Katika wilaya ya Mbozi Wanyiha wengi hupatikana magharibi, hasa vijiji vya Itaka, Nambizo, Mbozi mission, Shiwinga, Igamba na maeneo mengine ya huko. Pia upande wa mashariki utawakuta katika vijiji vya Nyimbili, Idiwili Hezya n.k.

Tena wako Zambia, Malawi na sehemu nyingine. Kwa jumla ni zaidi ya 600,000.

Inasadikiwa Wanyiha ni moja ya makabila ya Kibantu yenye asili ya Afrika Kusini (Wazulu au Wangoni).

Lugha yao ni Kinyiha. Kabila hili katika utamkaji wa maneno hufanana sana na Wasafwa, Wamalila, pia Wanyamwanga.

Wanyiha ni wapole na wasikivu. Baadhi ya koo za Kinyiha ni Mwashiozya, Mwashiuyà, Mwembe, Nzunda, n.k. Chifu wa Wanyiha ni Mwene.

Wanyiha wamezungukwa na makabila mbalimbali wakiwemo Wasafwa, Wandali, Wanyakyusa, Wabungu na Wanyamwanga.

Wanyiha walio wengi ni wakulima: zao kuu la chakula ni mahindi wakati zao kubwa la biashara ni kahawa.

wanyiha wanaposalimiana husema: Mwakataa... Halafu mtu wa pili hujibu: Ena..kabila hili wao huamini mgeni wa jirani ni mgeni wa wote .


Previous Page Next Page






شعب نيها ARZ Νυίχα Greek Nyiha people English

Responsive image

Responsive image