Waraka kwa Filemoni ni barua ambayo Mtume Paulo akiwa kifungoni (labda Efeso mwaka 56 au 57) alimuandikia mfuasi wake Filemoni. Ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vinavyounda Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Tofauti na barua zote zilizotangulia, hiyo haikuandikwa kwa kanisa fulani, bali kwa Mkristo binafsi, tajiri, pengine wa Kolosai.
Ingawa si muhimu upande wa teolojia, inaonyesha upendo wa mtume kwa wale aliowaongoa, na jinsi udugu wa Kikristo ulivyoanza kutikisa utumwa.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.