Washubi ni kabila mojawapo kati ya makabila ya Mkoa wa Kagera, nchini Tanzania. Washubi wamechanganyika na Watanzania wengine na, ukiacha sehemu kubwa ya kabila hili ambao wanaishi katika Wilaya ya Ngara, wanapatikana kwenye maeneo mengine nchini Tanzania wakijitafutia riziki na ustawi kwa njia moja au nyingine.
Kabila hili linaongea lugha ya Kishubi ambacho ni Kibantu ingawa Washubi si wote Wabantu. Washubi wanaweza kuelewana lugha na majirani zao Wanyambo, Wahaya, Wazinza na Walongo na kwa kiasi fulani makabila mengine ya maziwa makuu, ukiacha baadhi ya makabila, kama vile Wasukuma na Wanyamwezi.
Mwaka 1987 idadi ya Washubi ilikadiriwa kuwa 196,000 [1]. Wanaoishi katika wilaya ya Biharamulo wanaitwa Wasubi, lakini tofauti ni ndogo sana.