Wasimbiti ni kabila la Tanzania kaskazini, jamii ya Wakurya, pia wamechanganyika na Wajaluo.
Wanaishi kando ya Ziwa Viktoria katika wilaya ya Rorya karibu na mpaka wa Kenya na wa wilaya ya Musoma mjini. Mto Mara unakata vijiji kama vile Kirumi, Kuruya, Mbatamo, Kinesi, Nyamaguku au Iryenyi.
Wasimbiti wenyewe wanakadiriwa kuwa watu 33,000 hivi, pamoja na vikundi walio karibu na kuelewana nao kilugha kama vile Wahacha, Wakine, Wakiroba, Wasurwa na Wasweta wako zaidi ya laki 1.