Wasongora (pia: Washongora, Wahuma) ni kabila linaloishi magharibi mwa Uganda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni mchanganyiko wa Wabantu na Waniloti.
Lugha yao ni Kisongora (wao wanasema Lusongora) ambayo inafanana na Kinyankore.
Tangu zamani ni wafugaji wa ng'ombe.
Leo wanakadiriwa kuwa 25,000 upande wa Uganda na wachache zaidi upande wa Kongo; wengi wao ni Wakristo.