Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Wayao (Tanzania)

Kinyago, Malawi

Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa.

Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao kati yao 1,000,000 wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1]

Wayao ni miongoni mwa Wabantu wanaopatikana katika mataifa kadhaa barani Afrika na kwa ujumla wao wameenea Malawi, Msumbiji na Tanzania katika mikoa ya Mtwara na Ruvuma.

Wakipatikana zaidi katika eneo kati ya Ruvuma na karibu na mto Lugenda kaskazini mwa Msumbiji.

Wanasifika sana kwa kuwa na utambulisho wenye nguvu wa kiutamaduni unaovuka mipaka.

Shughuli yao kubwa ni kilimo cha hapa na pale.

Upande wa lugha Wayao wenyewe wanaongea Kiyao; vilevile wanazungumza lugha rasmi ikiwamo ile ya Kiswahili kwa wale waliopo Tanzania, Kiingereza kwa wale wa Malawi na Tanzania na Kireno kwa wale waliopo nchini Msumbiji.

Wengi wao ni waumini wa dini ya Uislamu.

Miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi: Bakili Muruzi pamoja na Joyce Banda.

  1. [1].

Previous Page Next Page






WaYao AF شعب ياو Arabic Яа BE Wa yao Catalan Wayao German Yao people (East Africa) English Jaoj EO WaYao Spanish Yao (Afrikako etnia) EU Yaot Finnish

Responsive image

Responsive image