Gairo ni wilaya mpya katika mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67700, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012. Hadi 2012 ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Kilosa.
Makao makuu ya wilaya yako Gairo, mji wenye maendeleo ya haraka.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012 kata ilikuwa na wakazi wapatao 193,011.[1] Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 258,205 [2].